Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood, Research Center cha
Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu (katikati), akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, akidai kutapeliwa na maofisa
wa jeshi la Magereza na Kujenga Taifa (JKT), katika utengenezaji wa
madawati ya bei nafuu kama Rais Dk. John Magufuli alivyoagiza.
Na Dotto Mwaibale, Dar
SHILINGI bilioni 6 zizotengwa na Rais Dk.John Magufuli kwa ajili ya
utengenezaji wa madawati zimeibua majipu katika Jeshi la Magereza na
Kujenga Taifa (JKT), kwa kudaiwa kumtapeli Mkurugenzi Mtendaji wa
Kiwanda cha Edosama Wood, Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es
Salaam, Edward Maduhu katika utengenezaji wa madawati.
Maduhu amezilalamikia taasisi hizo za jeshi akidai zimemtapeli katika
kazi ya kutengeneza madawati hayo baada ya kukubaliana kufanya
ushirikiano wa kazi hiyo kufuatia wao kuelemewa.
Maduhu alitoa lawama hizo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu kutapelewa na majeshi hayo waliofika
kiwandani kwake kuomba ubia wa kushirikiana kutengeneza madawati ya bei
nafuu kama alivyoagiza Rais.
Hata hivyo, Mkuu wa Kiwanda cha Magereza, ACP Ismail Mlawa, alisema
baada ya serikali kutoa ‘order ya kutengeneza madawati hao, taasisi hizo
mbili ziliunda timu maalumu ya kutengeneza madawati hayo.
Alisema, baada ya kuunda timu hiyo, walikubaliana kuzunguka kwenye
viwanda mbalimbali nchini kwa ajili ya kuangalia vifaa na sampuli ya
utengenezaji wa madawati hayo ili yaweze kuwa katika ubora unaokubalika.
Alisema, kutokana na hali hiyo, timu hiyo ilikwenda kwenye viwanda
mbalimbali kikiwamo hicho cha Edosama kwa lengo la kuangalia upatikanaji
wa vifaa na si vinginevyo.
“Tulienda kwenye viwanda zaidi ya vinne kikiwamo cha Edosama, lengo ni
kuangalia namna ya upatikanaji wa ‘material’ (vifaa) vya kutengeneza
madawati pamoja na kufanya ‘window shoping’ lakini katika viwanda vyote
hivyo, hakuna hata kimoja tulichoingia nacho mkataba wa kutengeneza
madawati kwa sababu hatukuwa na mamlaka ya kufanya hivyo mpaka
tutakapowasilisha taarifa kwa viongozi wetu,”alisema Mlawa.
Aliongeza, baada ya kuona wanavyotengeneza madawati hao, walilazimika
kuwasilisha taarifa hiyo kwa viongozi wao ili waweze kujadiliana
kuhusiana na suala la utengenezaji wa madawati hao.
Maduhu alisema Aprili 12 mwaka huu walipigiwa simu na maofisa wa Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza ambao walifika katika
kiwanda chao na kufanyanao vikao vinne kuanzia Aprili 12 na 15 mwaka
huu.
Alisema maofisa wa majeshi hayo walioshiriki vikao hivyo ni Kanali
Wanyancha na Tendwa Mahunnah wote kutoka JKT na ASP Mlawa pamoja na
ofisa mwingine wa Jeshi la Magereza ambaye jina lake halikupatikana.
Maduhu alisema kwamba katika kikao hicho jumla walikuwa saba pamoja na
maofisa wa kiwanda hicho na kuwa katika kikao hicho walifanikiwa kupiga
picha za mnato, kurekodi mazungumzo yote.
Aliongeza kuwa katika kikao hicho maofisa hao wa jeshi waliwaeleza kuwa
wamefika kiwandani hapo baada ya kushindwa bei ya madawati iliyotolewa
na Rais ya sh.50,000 kwa kila dawati kwani gharama zao za kutengeneza
dawati moja ni zaidi ya sh.78,000.
Alisema kwamba katika kikao hicho walikubaliana kiwanda hicho kipewe
kazi ya kusambaza vyuma vya miguu ya madawati hayo vyenye ukubwa wa
inchi 1x1-1.5 mm vikiwa vimepakwa rangi.
Maduhu alisema baada ya kukubaliana walianza kuwapa teknojia ya
utengenezaji wa madawati hayo huku wakiendelea kuandika hadi
waliporidhika na gharama ya kutengeneza dawati moja kwa sh.38,000 na
sh.40,000 kwa teknolojia ya kiwanda hicho.
Alisema baada ya kupata teknolojia hiyo walikata mawasiliano na kila
walipokuwa wakiwapigia simu walikuwa hawapokei.
Alisema kiwanda hicho kimetumia zaidi ya sh.bilioni moja kwa ajili ya
utafiti wa miaka mitano kwa kutembea viwanda katika nchi 17 ili
kujifunza teknolojia hiyo na kuwa wao wamekuwa wa kwanza kubuni aina
mpya za madawati hapa nchini.
HABARI
HABARI
MICHEZO
‹
›
BURUDANI
BURUDANI
BURUDANI
BURUDANI
BURUDANI
BURUDANI
SIASA
VIDEOZ
»
Previous
This is the last post.
Elekezo: HABARI
»
Previous
This is the last post.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments