http://sufianimafototest.blogspot.com/
http://sufianimafototest.blogspot.com/
http://sufianimafototest.blogspot.com/
http://sufianimafototest.blogspot.com/
http://sufianimafototest.blogspot.com/

HABARI

HABARI

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

BURUDANI

BURUDANI

BURUDANI

BURUDANI

SIASA

VIDEOZ

» » Yanga Yazidi Kuukaribia Ubingwa, Yawachapa Stand United Kwao Mabao 3-1
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post





YANGA leo imezidi kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuzidi kuwa na matumaini ya kutetea ubingwa wao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga jioni ya leo.
Katika mchezo huo wa leo ni wachezaji waKimataifa Donald Ngoma na Amis Tambwe walioiangamiza Stand huku Ngoma akitupia mabao mawili na Tambwe akitupia bao moja na kufikisha jumla ya mabao 20 katika mbio za kuwania ufungaji bora.
Baada ya mchezo wa leo Yanga sasa imefikisha jumla ya Pointi 68 wakiwa tayari wamecheza jumla ya mechi mechi 27, ambapo mchezo unaofuata ni kati yao na Mbeya City unaotarajia kupigwa baada ya mchezo wao wa kimataifa.

Yanga sasa inaweza kutangaza ubingwa ndani ya mechi mbili zijazo kati ya tatu za mwisho, iwapo itaendeleza wimbi la ushindi. 
Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, Yanga tayari walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma.
Ngoma alifunga bao la kwanza katika dakika ya pili kwa shuti kali, baada ya kuupitia mpira kwenye himaya ya mabeki wa Stand, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Assouman David.  
Ngoma tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 45 kwa bao zuri akimlamba chenga kipa wa Stand United, Frank Muwonge baaada ya kutanguliziwa pasi nzuri na Mrundi, Amissi Tambwe.

Kipindi cha pili, Yanga ilifanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na Tambwe dakika ya 63 akimalizia kona ya winga Simon Msuva. 
Kwa upande wa Stand, Elias Maguri akaifungia bao la kufutia machozi katika dakika ya 82 baada ya kiungo wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kumchezea rafu kiungo wa Stand, Suleiman Kassim 'Selembe'.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

TOA MAONI